BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Shinyanga
HUKUMU ya kesi ya shambulizi la kudhuru mwili anayodaiwa kufanyiwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Mwanahiba Richard dhidi ya kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto imetolewa leo huku mahakama ikimuachia huru mchezaji huyo baada ya kuonekana hana hatia.

Mwanahiba alidai kushambuliwa na Mwinyi Februari 10, baada ya mazoezi ya timu hiyo ilipokuwa inajiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United, mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga iliongozwa na Hakimu Mfawidhi, Rahim Mushi ambapo wahusika wa kesi hiyo Mwinyi na Mwanahiba wote walikuwepo wakati hukumu hiyo inasomwa.

Hii ilikuwa ni mara ya tano ambapo awali ilitajwa tu lakini leo ilisomwa hukumu huku baada ya juzi mtuhumiwa kupewa nafasi ya kujitetea wakati mlalamikaji naye alijieleza.

Mahakamani hapo leo Mwinyi aliongozana na mwanasheria wake Kaunda wakati Mwanahiba alikuwa na mwanasheria wa serikali Upendo Shemkole.

Hata hivyo, baada ya kusomwa hukumu hiyo, hakimu Mushi alitoa muongozo kuwa upande wa mlalamikaji unaweza kukata rufaa kama hawakuridhishwa na maamuzi ya mahakama hiyo.

BOIPLUS ilimtafuta Mwanahiba ambaye alisema "Mimi sina maamuzi yoyote, kampuni yangu ndiyo yenye mamlaka katika hili, kwahiyo labda wao ndio wanaweza kusema kama tutakata rufaa au vipi.

Post a Comment

 
Top