BOIPLUS SPORTS BLOG

 Leseni za wachezaji Juma Mahadhi na Hassan Kessy

LICHA ya Shirikisho la soka Barani Afrika CAF kutoa leseni kwa wachezaji wanne wapya wa Yanga, wachezaji hao hawataruhusiwa kucheza mchezo wao dhidi ya MO Bejaia hadi hapo klabu zao za zamani zitakapotoa barua za kuwaruhusu.

Wachezaji hao wapya ambao tayari kocha Han Pluijm ameshawaingiza katika programu yake ni Hassan Kessy, Andrew Vicent 'Dante', Juma Mahadhi na Benno Kakolanya. 

Afisa mmoja wa CAF aliiambia ABM FM Radio kuwa; "Ili wachezaji walioongezwa na Yanga wacheze mechi ya kesho ni lazima timu walizokuwa wakichezea zitoe barua ya kueleza kuwa hawana pingamizi, vinginevyo hawatoruhusiwa kucheza."

Benno, Dante na Mahadhi ni wachezaji huru na kwamba uhamisho wao ulishakamilika kwenye mfumo wa kielektroniki (TMS), hofu ipo kwa Kessy ambaye alisajiliwa na Yanga baada ya kusimamishwa na Klabu yake na inaelezwa kuwa mkataba wake unamalizika mwezi huu hivyo ni lazima viongozi wa Simba wakubali uhamisho huo kwenye mtandao.

Viongozi wa Simba wamenukuliwa wakikiri kupokea taarifa hizo lakini wamekosa jinsi ya kuwasaidia watani zao kwavile taarifa zimewafikia jioni na kesho ni siku ya mapumziko.

Kama suala hilo halitapatiwa ufumbuzi, Pluijm atalazimika kumtumia Mbuyu Twite katika nafasi ya beki wa kulia ambako alimuandaa Kessy kuziba pengo la Juma Abdul ambaye ni majeruhi.


           Leseni za Kakolanya na Dante

Post a Comment

 
Top