BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
LESENI za wachezaji wanne wapya waliosajiliwa na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga zimetumwa na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF.

Wachezaji waliotumiwa leseni hizo ni Hassani Kessy,Beno Kakaolanya, Andrew Vincent na Juma Mahadhi ambao sasa wanaweza kuitumikia Yanga katika michuano ya ndani na nje.

Ofisa Habari wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania  TFF, Alfred Lucas amethibitisha kupokea leseni hizo toka CAF na kusema kuwa wachezaji hao wanaweza kuitumikia klabu hiyo katika michuano mbali mbali.

"Ni kweli tumepokea leseni za wachezaji hao toka CAF zinazowawezesha kuitumikia klabu hiyo katika michuano ya ndani na nje" alisema Alfred.

Wachezaji hao walisafiri na kikosi cha Yanga kilichokwenda kuweka kambi nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.

Yanga itasafiri kesho kutoka Uturuki kuelekea Algeria tayari kwa mtanange huo utakaopigwa siku ya Jumapili.

Post a Comment

 
Top