BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu

TIMU ya TP Mazembe imetua usiku huu kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam huku wakitamba kuwa wamekuja kuchukua pointi tatu dhidi ya Yanga, jumanne hii.

Kipa na nahodha wa timu hiyo, Muteba Kidiaba alisema kuwa wanakuja wakitambua ugumu wa mechi hiyo lakini wana uhakika wa kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo.
"Yanga ni timu nzuri na ndio maana imefika kwenye hatua kama hii lakini tutatumia uzoefu wetu tulionao kupata pointi tatu dhidi yao," alisema Kidiaba.

Timu hiyo imekuja na msafara wa watu 32 ambao ni wachezaji  18 na maofisa 14.

Post a Comment

 
Top