BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar
YANGA imemsajili kipa kutoka Prisons ya jijini Mbeya, Beno Kakolanya ambaye ameweka wazi kuwa hii ndiyo mara yake ya kwanza kukwea pipa (Ndege) tangu aanze kucheza Ligi Kuu Bara ambapo sasa yupo Uturuki ambako Yanga wamepiga kambi yao.

Yanga inajiandaa na mechi yao ya kimataifa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi ambapo watacheza na Bejaia Juni 17 nchini Algeria.

Akizungumza na BOIPLUS kutoka kambini huko, Beno alisema kuwa katika maisha yake ya soka aliwaza kucheza timu kubwa ambapo ndoto imetimia ila kutoka nje ya Tanzania hii ni mara yake ya kwanza.

''Toka nianze kucheza ligi sijawahi kutoka kwenda kucheza mechi za kimataifa na sijawahi kutoka nje ya nchi ndo mara kwanza, hivyo nitapambana kwa kadri niwezavyo, kwani naona kabisa maisha ndani ya Yanga ni mazuri,'' alisema Beno

Yanga imesafiri na wachezaji wake wote wapya akiwemo Hassan Kessy, Juma Mahadhi na Andrew Vincent 'Dante'.

Naye Meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe alisema kuwa: ''Kambi iko salama kabisa na hakuna mchezaji mwenye matatizo hata hawa wapya wameanza kuzoea maisha ya Yanga,''

Post a Comment

 
Top