BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

VIINGILIO vya mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika baina ya Yanga na TP Mazembe vimetangazwa ambapo kiingilio cha chini ni shilingi 7000 na cha juu ni 30,000.

Viingilio hivyo vimepangwa kama ifuatavyo VIP A ni shilingi 30,000 VIP B na C ni shilingi 25,000 huku machungwa, Kijani na manjano ikiwa ni shilingi 7000.

Ofisa Habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro amewataka wapenzi na wanachama wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuongeza hamasa kwa wachezaji ili kuweza kuibuka na ushindi katika mtanange huo.

Straika mtanzania, Thomas Ulimwengu anayeitumikia YP Mazembe ya DRC

"Tunawaomba wapenzi na wanachama wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuishaingilia timu kwakuwa tunahitaji sana uwepo wao kulingana na ukubwa wa mechi ambapo ushindi pekee ndiyo utatuweka katika nafasi nzuri," alisema Jerry.

Katika hatua nyingine kikosi cha mabingwa hao kimerejea nchini kikiwa kamili  na tayari kipo kambini kuivutia kasi TP Mazembe ambayo katika mchezo uliopita ilishinda magoli 3-1.

Yanga itashuka dimbani siku ya Jumanne katika uwanja wa Taifa saa 10 jioni kuwakabili mabingwa hao wa kihistoria barani Afrika.

Post a Comment

 
Top