BOIPLUS SPORTS BLOG

LEICESTER, Uingereza
MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Leicester City, Aiyawatt Srivaddhanaprabha​ anaamini mshambuliaji wao anayewindwa na  Arsenal Jamie Vardy ataendelea kusalia  Kings Power msimu ujao baada ya kuipiga chini ofa ya Washika bunduki hao.

Arsenal walipeleka ofa ya pauni 20 milioni ambayo walikuwa na matumaini ya kukamilisha dili hilo kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016. Vardy alichelewa kutoa maamuzi hadi itakapomalizika michuano na sasa klabu yake imempandishia mshahara hadi pauni 100,000 kwa wiki sawa na ambao angelipwa Arsenal.

Akizungumza na gazeti la  Mail, Makamu huyo alisema hatma ya mshambuliaji huyo itajulikana muda mfupi ujao na ana uhakika wa kumbakiza mpachika magoli huyo aliyetisha msimu uliopita.

"Mtapata habari muda si mrefu, lakini nina imani atabaki.
Tunataka kujenga kikosi bora msimu ujao kitakacho washangaza wengi kuanzia kwenye ligi na klabu bingwa.

"Michuano ya klabu bingwa tumepania kufanya vizuri japokuwa wengi wanatuona kama ni wachanga, na hatutishiki na uchanga wetu," alimaIizia Aiyawatt.

Post a Comment

 
Top