BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa
KATIKA michuano ya bara la ulaya inayo tarajiwa  kufunguliwa kwa mchezo   baina ya mwenyeji   Ufaransa dhidi ya Romania usiku wa leo, kuna mkusanyiko wa vipaji kutoka klabu mbalimbali barani Ulaya, hizi hapa ni klabu nane zinazo ongoza kuwa na wachezaji wengi katika michuano hiyo.

LIVERPOOL ( UINGEREZA) 12
 Liverpool ikiwa na wachezaji 12 wanaoshiriki UEFA EURO 2016 ina wachezaji watano kutoka  katika kikosi cha England ambao ni James Milner, Adam Lallana, Nathanael Clyne, Jordan Henderson na  Daniel Sturridge. Wengine ni Joe Allen na Kipa Dany Ward wanao wakilisha taifa la Wales.

 Pia Liverpool inao wawakilishi kutoka taifa la Ubelgiji ambao ni Simon Mignilet, Christian Benteke na Divock Origi, wengine ni Emre Can (Ujerumani) na  anayekamilisha idadi ya 12 ni Martin Skrtel( Slovakia)

JUVENTUS (ITALIA) 12
Juventus  nao wana idadi sawa na majogoo wa Anfield, Liverpool  kwakuwa na wachezaji wengi katika michuano ya Euro. Nusu ya wachezaji wa Juventus walio katika michuaano ya Euro 2016 wanawakilisha Italia amabao ni Giuling Buffon, Giorgio Chiellin, Simon Zaza, Stefano Stuaro, Andrea Bazagrina na Leonardo Bonnucci. Huku Poul Pogba na Patrice Evra wakiwakilisha Ufaransa na wengine wanaokamilisha idadi  ya 12 ni Stephen Lichesteiner (uswis), Sami Khedira (Ujerumani), Alvaro Morata (Hispania) na Mario Mandzudic (Crotia).

TOTENHAM  HOTSPURS (UINGEREZA) 11
Totenham ni klabu iliyofanya vizuri sana msimu huu katika ligi kuu Uingereza ikiwa na kikosi cha wachezaji makinda wengi kilichoibuka nafasi ya pili na katika michuano ya UEFA EURO mwaka huu wanawakilishwa na wachezaji 11 ambao watano kati ya hao watavaa jezi za Waingereza ambao ni mabeki Kyle Walker, Danny Rose na viungo  ni Delle Alli na Eric Dier huku mshambuliaji akiwa Harry Kane. 

 Wengine ni Mousa Dembele, Jan Vetonghan na Toby Anderweired wakiwakilisha  Ubeligiji na kipa wao atakuwa mwenyeji wao kule Ufaransa akiwa na timu yake ya Ufaransa (Hugo Lloris)

MANCHESTER UNITED (UINGEREZA) 10 
Mashetani wekundu kutoka Manchester wao wapo katika nafasi ya nne kati ya timu zenye wachezaji wengi EUFA EURO 2016. Wachezaji hao ni Chris Smalling , Wyne Rooney na Marcus Rashford ambao wao wanawakilisha Waingereza, Morgan Schneiderlin na Anthony Martial wakiwakilisha  Ufaransa .


Wengine ni Bastian Schweinsteiger(Ujerumani),  Paddy MC Nair (Nothern Ireland), David De Gea (Hispania) , Fellain ( Ubelgiji) na anaekamilisha idadi ya wachezaji 10 ni Matteo Darmian.

Klabu  nyingine  zenye wachezaji wengi  katika michuano ya Euro mwaka huu zimefungana katika nafasi ya tano ambazo kila klabu ina wachezaji tisa katika michuano hiyo na hizo klabu  ni  Barcelona (Hispania), Fenabarhce ( Uturuki), Bayern Munchen (Ujerumani) na mwisho Shakhtarn Donestk ( Ukraine)  

Post a Comment

 
Top