BOIPLUS SPORTS BLOG

Madrid, Hispania

KIUNGO wa Juventus na timu ya Taifa ya Ufaransa  Paul Pogba yuko mbioni kujiunga na mabingwa wa kihistoria wa klabu bingwa barani Ulaya   Real Madrid kwa dau la pauni milioni 60

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na kujiunga na Manchester united lakini wakala wake Mino Raiola alinukuliwa akisema Madrid wako tayari kumlipa Pogba pauni 135,000 kwa wiki na kuongezeka hadi pauni 200,000.

Kiungo huyo wazamani wa United amekuwa akihitajika sana na Rais wa klabu hiyo  Florentino Perez ambaye anajua atapata upinzani mkubwa toka kwa meneja wake wa zamani  Jose Mourinho aliyejiunga na Mashetani Wekundu mwezi uliopita.

Tangu kuwasili kwa Mreno huyo  Old Trafford, kumeripotiwa kuhitaji huduma ya Mfaransa huyo ili kuimarisha safu ya kiungo ambayo imekuwa iliyumba sana msimu uliopita.

Pogba anaiwakilisha Ufaransa katika michuano ya Euro inayofanyika nchini humo na kuisaidia kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Romania katika mchezo wa ufunguzi siku ya Ijumaaa.

Post a Comment

 
Top