BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro John Mabula.

 Mbali ya Mtibwa Sugar, taarifa za Mabula ambaye pia amewahi kuchezea Moro United ya Morogoro na Shinyanga Shooting ya Shinyanya kwa mafanikio katika nafasi ya ulinzi kwa muda mrefu  aliuawa kwa kuchomwa kisu na mwenzake alipokuwa akiamulia ugomvi huko Kitunda nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Rais  Malinzi amemwelezea Mabula kuwa ni mchezaji aliyekuwa na uwezo na uadilifu na mchango wake katika soka utabaki katika dhana ya kumbukumbu ya wachezaji mahiri wa Tanzania waliotokea kucheza nafasi ya ulinzi.

Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa uongozi wa timu alizowahi kuchezea ambazo ni Mtibwa Sugar, Moro United na Shinyanga Shooting. Kadhalika familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata pia kucheza timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ mwaka 2002-2004.

Malinzi amewaasa wadau wote kuwa watulivu wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wetu Mabula hasa kutokana na mazingira ya kifo.

 Bwana alitoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amina.

Post a Comment

 
Top