BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Dar
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Yussuf Manji kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Yanga baada ya kupata kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku Kura mbili zikiharibika.

Malinzi pia amempongeza Clement Sanga kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti  baada ya kupata kura 1,428 wakati mpinzani wake Titus Osoro alipata kura 80.


 Kadhalika wajumbe wanane wanaounda Kamati ya Utendaji kwa kuchaguliwa kuongoza Klabu ya Yanga kwa miaka minne ijayo kwa mujibu wa katiba.

Wajumbe waliochaguliwa ni Omary Said (1,069), Siza Lyimo (1,027), Salum Mkemi (894), Thobius Lingalangala (889), Ayoub Nyenzi ((889), Samwel Lukumay (818), Hussein Nyika (770) na Hashim Abdallah (727.

 Katika salamu hizo za pongezi, Rais  Malinzi pia amewapongeza wanachama wa Yanga kwa kufanya uchaguzi wa amani na utulivu.

 Kutokana na hali hiyo Malinzi ameutaka uongozi huo wa kufungua ukurasa mpya wa kuendesha klabu hiyo ili kuiletea mafanikio na kuepuka marumbano yasio na msingi kitu ambacho kitaharibu taswira nzima ya Yanga.Post a Comment

 
Top