BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
MANCHESTER City ipo katika mazungumzo na Borussia Dortmund kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji  Pierre-Emerick Aubameyang.

Aubameyang ndiye mchezaji bora wa mwaka wa Bundesliga pia amekuwa akihusishwa kujiunga na mabingwa wa kihistoria wa Ulaya Real Madrid msimu huu lakini City wapo katika nafasi nzuri ya kumnyakua Mgabon huyo.

Mshambuliaji huyo amefunga magoli 25 katika michezo 29 akizidiwa na Straika wa Bayern Munich  Robert Lewandowski pekee.

Endapo City watafanikiwa kumpata atakuwa mchezaji mwingine toka Borrusia Dortmund baada ya kocha wao Pep Guardiola kumsainisha kiungo  Ilkay Gundogan wiki iliyopita.

Beki Aymeric Laporte anayekipiga Athletic Bilbao na John Stones wa Everton pia Guardiola amekuwa akiwahitaji kuimairisha safu ya ulinzi.

Post a Comment

 
Top