BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester United imekamilisha usajili wa beki Erick Bailly toka Villareal kwa ada ya pauni 31 Milioni.

Beki huyo alifaulu vipimo vya afya jana Jumanne na leo amesaini kandarasi ya miaka minne itakayomuweka klabuni hapo hadi mwaka 2020.

Huu ndiyo usajili wa kwanza wa kocha Jose Mourinho tangu alipochukua kibarua cha kunoa timu hiyo baada ya kufungashiwa virago Mdachi Luis van Gaal mwezi uliopita.

Bailly raia wa Ivory coast alinukuliwa akisema "Ndoto zimekuwa kweli nimekuja kwenye timu ambayo nilikuwa naipenda tangu utotoni".

Bailly ataongeza nguvu katika safu ya ulinzi ya United ambayo imekuwa ikimtegea Chris Smalling kama beki wa kati na sasa ataungana na nyota huyo aliyejengeka kimazoezi.

Licha ya uimara mkubwa aliokuwa nao Bailly lakini tatizo lake kubwa ni nidhamu ndani ya uwanja ambapo msimu huu ameoneshwa kadi za njano 10 huku alitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali wa Europa ligi dhidi ya Valencia.

Post a Comment

 
Top