BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Diamond Jubilee, Dar
Mwenyekiti mteule, Yusuph Manji

HATIMAYE asubuhi hii klabu ya Yanga imemaliza salama ule mchakato wa kupata viongozi wapya watakaoiongoza kwa miaka minne ijayo.

Mwenyekiti Yusuph Manji ambaye hakuwa na mpinzani katika nafasi hiyo ametangazwa mshindi baada kuonyesha kuaminiwa sana na wanachama kwa kupata kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zikiharibika na hakukuwa na kura ya hapana.

Clement Sanga ambaye alikuwa akipambana na Titus Osoro, ameibuka mshindi katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti baada ya kujizolea kura 1,428 kati ya 1,508 zilizopigwa. Mpinzani wake aliambulia kura 80 na hakukuwa na kura zilizoharibika.


Makamu Mwenyekiti mteule, Clement Sanga

Katika nafasi ya Wajumbe wa kamati ya Utendaji, kulikuwa na wagombea 20 huku wanane waliopata kura nyingi ndio wametangazwa kuunda kamati hiyo yenye maamuzi ndani ya klabu.

Wagombea walioibuka kidedea katika nafasi hiyo na kura zao katika mabano ni;
1. Siza Augustino Lymo (1027)
2. Omary Said Amir (1069)
3. Tobias Lingalangala (889)
4. Salim Mkemi (894)
5. Ayoub Nyenzi (889)
6. Samuel Lucumay (818)
7. Hashim Abdallah (727)
8. Hussein Nyika (770)


Bakari Malima 'Jembe Ulaya' amebwagwa katika kinyang'anyiro hicho

Wagombea ambao kura zao (kwenye mabano) hazikutosha ni;
1. David Luhago (582)
2. Godfrey Mheluka (430)
3. Ramadhani Kampira (182)
4. Edgar Chibura (72)
5. Mchafu Chakoma (69)
6. George Manyama (249)
7. Bakari Malima (577)
8. Lameck Nyambaya (655)
9. Beda Tindwa (452)
10. Athumani Kihamia (558)
11. Pascal Lizer (178)
12. Silvester Haule (197)

Post a Comment

 
Top