BOIPLUS SPORTS BLOG

London, Uingereza
KLABU ya Arsenal ipo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy kwa ada ya pauni milioni 20.

Mshambuliaji huyo ambaye alifunga magoli 24 katika mashindano yote msimu uliopita aliisaidia timu yake kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo ambaye alisaini mkataba mpya na timu yake anaolipwa pauni 70,000 kwa wiki na sasa akijiunga na washika bunduki atalipwa pauni 120,000.

Kocha wa Leicester Claudio Ranieri alithibitisha kufikia muafaka na Arsenal juu ya mshambuliaji huyo ambaye yupo kambi ya timu ya Taifa kuelekea michuano ya Euro utakaopigwa nchini Ufaransa.

Taarifa zinasema Vardy atafanyiwa vipimo vya afya leo na kusaini mkataba kabla ya kesho kusafiri na 'Three Lions' kuelekea Ufaransa.

Kocha wa Uingereza Roy Hogson amesisitiza dili hilo likamilike kabla timu hiyo haijasafiri kwenda kwenye michuano ya Euro ili kuleta utulivu ndani ya kikosi.

Post a Comment

 
Top