BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

MASHABIKI 500 toka Jamhuri ya kidemokrasia Congo watakuja kuishangilia timu ya TP Mazembe katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi Yanga mtanange utakaopigwa kesho katika uwanjani wa Taifa jijini Dar es Salaam saa 10 jioni.

Tayari mashabiki hao wameanza safari ya kutoka Congo kwa usafiri wa mabasi na wanatarajiwa kufika nchini usiku wa leo kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro.

"Wanakuja na mashabiki 500 na hivi tunavyozungumza wapo safarini kwa njia ya barabara, kuhusu utaratibu wa wao kukaa pale uwanjani tayari ulishaandaliwa," alisema Jerry.


Uongozi wa Yanga jana ulitangaza kufuta viingilio katika mchezo huo ili kuwezesha mashabiki wengi kujitokeza kuwapa nguvu mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara.

Aidha Muro aliwataka mashabiki watakaofika uwanjani kuvaa jezi za timu hiyo ili kuongeza msisimko wa mchezo ambao unatabiriwa kuwa mgumu kutokana na uimara wa timu zote.

Katika mchezo wa awali dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria Yanga ilipoteza    ugenini kwa goli 1-0 na hivyo kutakiwa kufanya kila linalowezekana kuibuka na ushindi katika mtanange huo.

Post a Comment

 
Top