BOIPLUS SPORTS BLOG

NEW JERSEY, Marekani

CHILE imefanikiwa kunyakua ubingwa wa kombe la Copa America kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kuifunga Argentina kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika dakika za kawaida usiku wa kuamkia leo.

Fainali hiyo inakuwa ni muendelezo wa kushindwa kuisaidia nchi yake ya Argentina kufanya vizuri katika michuano mikubwa kwa mchezaji bora wa dunia mara tano Lionel Messi baada ya mwaka jana pia kupoteza.

Katika fainali hiyo Messi alikosa mkwaju wa penalti na kudidimiza matumaini ya kufikia rekodi ya kumfikia gwiji Diego Maradona kutokana na kuifanya makubwa nchi yake.

Argentina wamepoteza fainali ya pili mfululizo mbele ya Chile huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa goli 1-0 katika fainali ya kombe la Dunia mwaka 2014 zilizofanyika nchini Brazil dhidi ya Ujerumani.


Argentina ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kunyakua kombe baada kuwa na nyota wengi kama Messi,Sergio Aguero, Angel Di Maria, Gonzalo Higuan lakini kwa mara nyingine wameangukia pua.

Messi mwenye umri miaka 29 amenyakua makombe yote katika ngazi ya klabu akiwa na Barcelona lakini katika timu ya Taifa mambo bado hayamuendei vizuri.

Wachezaji wengine waliokosa penalti ni Lucas Biglia huku Artulo Vidal akikosa penati kwa upande wa Chile.

Post a Comment

 
Top