BOIPLUS SPORTS BLOG

PHOENIX, Marekani
BINGWA wa zamani wa dunia wa masumbwi uzito wa juu, Muhammad Ali amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74.

Bingwa huyo aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la upumuaji alifariki katika hospitali ya US City of Phoenix iliyopo jimbo la Arizona baada ya kulazwa siku ya Alhamisi.

Msemaji wa Familia alisema Ali alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo muda mrefu huku hali yake ikibadilika mara kwa mara.

Ali atakumbukwa na wadau wengi wa masumbwi hasa katika pambano dhidi ya Sony Liston mwaka 1965 baada ya kumchapa kwa 'Knockout' ndani ya sekunde moja.

Katika mipambano yake ya kimataifa Ali aliahinda 51 huku 37 ikiwa ni Knockout.

Bingwa huyo atazikwa nyumbani kwao Louisville Kentucky tarehe ambayo itapangwa.

Post a Comment

 
Top