BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
WAZIRI wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amewataka watanzania kuendelea kuiunga mkono Taifa Stars licha ya kutolewa katika michuano ya AFCON ambayo fainali zake zitafanyika mwakani, Gabon.

Nape alikuwa mgeni rasmi katika mchezo kati Taifa Stars dhidi ya Misri na kushuhudia vijana wake wakikubali kichapo cha bao 2-0 na kufuta  matumaini ya Stars kucheza fainali hizo.

Nape alisema kuwa Stars walipambana kwa uwezo wao lakini walikutana na timu yenye uwezo zaidi ndiyo sababu ya kupoteza mechi nyumbani japokuwa wangeweza kubadili matokeo.

"Lazima tukubali kuwa Misri ni bora zaidi yetu wachezaji wao wana uzoefu mkubwa na michuano hii ila na sisi tulicheza vizuri lakini muunganiko wa timu haukuwa mzuri," alisema Nape

Kuelekea mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Nigeria utakaofanyika Septemba, Waziri huyo alisema timu inabidi ifanye maandalizi mapema ili kuweza kuwakabili wenyeji ambao nao wameshindwa kufuzu.

Misri ndiye kinara wa kundi G baada ya kujikusanyia pointi 10 na kufuzu moja kwa moja kutokana na wapinzani wake kushindwa kuzifikia pointi hizo hata wakishinda katika mchezo wa mwisho.

Post a Comment

 
Top