BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar

BEKI wa zamani wa Simba raia wa Burundi, Emery Nimubona ameingia jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo kwa ajili ya kuja kutafuta timu ya kuichezea msimu ujao.

Nimubona aliachwa na Simba mara baada ya kumalizika kwa msimu uliopita kwa madai ya kushindwa kuonyesha kiwango kizuri na alirejea nchini kwao huku akiweka wazi kuwa ataangalia uwezekano wa kupata timu nchini Burundi, Rwanda au Kenya.

Akizungumza na BOIPLUS  Nimubona alisema amekuja kufanya mazungumzo na timu ambayo hakutaka kuitaja jina kwavile bado hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa.

"Ni kweli nimerudi Tanzania, kuna timu nazungumzanayo ingawa sitokutajia hadi hapo mipango itakapokaa sawa. Kama hatutokubaliana basi nitatafuta timu nyingine hapa hapa nchini," alisema Nimubona.

Timu za ligi kuu zimeanza kupigana vikumbo kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom.

Post a Comment

 
Top