BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
 Nahodha wa Stars, Mbwana Samatta (10) akitafuta mbinu za kumtoka beki Andrew Vicent kushoto. Stars inajiandaa na mchezo dhidi ya Misri hapo kesho. Wakishinda mchezo huo wataamsha matumaini ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika

 Straika wa Stars anayeichezea TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu akichuana na kiungo Hassan Kabunda 

 Juma Abdul anategemewa kuanzisha mashambulizi kupitia upande wa kulia, beki huyo amekuwa katika kiwango bora kutokana na uwezo wake wa kupanda na kupiga krosi

 John Bocco amekuwa hana bahati sana na timu ya Taifa licha ya kufanya vizuri mazoezini, je kesho atafanikiwa kufuta historia mbaya?

 Vita ya viungo wa kati, Himid Mao na kinda Juma Mahadhi

 Fundi Ibrahim Ajib akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji anayekuja kasi, Jeremia Juma (kushoto) huku kisiki David Mwantika akiwa tayari kutoa msaada


 Kocha wa makipa Peter Manyika akitoa maelekezo kwa makipa wa Stars Deogratius Munishi 'Dida', Benno Kakolanya na Aishi Manula

 Kiungo Jonas Mkude akiwa ndani ya Basi tayari kurejea Hotelini ambako wachezaji watapumzika hadi kesho kabla hawajaingia katika dimba la Taifa kuitetea Bendera ya Taifa "Usihofu, Misri lazima wakae kesho...", Samatta akionyesha kujiamini sana kuelekea mchezo wa kesho

 Straika Elius Maguri aliifungia Stars bao pekee dhidi ya Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki, je kesho ataendeleza moto wake?

 Wachezaji na makocha wa Stars wakifanya dua mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya mwisho leo

Kiatu anachokitumia Samatta mazoezini 'S77'

Post a Comment

 
Top