BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
STRAIKA wa KRC Genk ya Ubelgiji na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta amekuwa nyota wa Tanzania ambaye amejizolea tuzo nyingi tangu aanze kufahamika. Mtandao wa BOIPLUS uliamua kumtembelea nyumbani kwake ili kujua anazihifadhi vipi tuzo na medali zote alizowahi kutunukiwa. Hizi hapa ni baadhi ya picha:


Ukifika tu nyumbani kwake utakaribishwa na kabati kubwa lililopambwa kwa medali, vyeti na tuzo mbalimbali alizowahi kutwaa mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba Sc na TP Mazembe ya DR Congo


Licha ya kutisha awapo uwanjani, kumbe Samatta ni mtaalamu wa matumizi ya kiofisi ya kompyuta. Hiki hapa ni cheti chake alichotunukiwa baada ya kuhitimu mafunzo hayo


Mara kadhaa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimekuwa kikimpatia tuzo Samatta kwa kuthamini mchango wake kwenye Tasnia ya michezo nchini, hiki hapa ni cheti alichotunukiwa na TASWA 2015


Katika msimu wa 2013/14, TASWA ilimtaja Samatta kama Mchezaji Bora anayecheza nje ya nchi. Na hii hapa ndio tuzo yake ambayo inapamba kabati lake pia


Mwishoni mwa mwaka jana, Samatta akiwa na TP Mazembe alishiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu huko Japan. Mazembe haikufanya vizuri lakini wachezaji walipewa tuzo za ushiriki ambayo inaonekana hapo juu


TASWA pia ilimpatia tuzo ya Mchezaji mwenye Mafanikio ndani ya miaka 10 kuanzia 2005 hadi 2015


Tuzo nyingine ambayo inapatikana ndani ya kabati la Samatta alipewa na mtandao wa GOAL.COM kama mchezaji bora wa mwaka 2014


2011 akiwa anaitumikia klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam alishiriki michuano ya Mapinduzi Cup na kufanikiwa kupata medali ya dhahabu.....nayo ilikutwa imehifadhiwa mahali pake ndani ya kabati


Mwaka jana ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Samatta, licha ya kuvaa medali ya dhahabu ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika, mkali huyo wa mabao aliyeanzia soka lake katika viunga vya Mbagala jijini Dar, alifanikiwa pia kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo


Hii ndio tuzo kubwa kabisa ya binafsi aliyowahi kutwaa Samatta, alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa wanaocheza ligi za ndani


Na hiki ni cheti kilichoambatana na tuzo hiyo ya Afrika


2010 Samatta aliungana na vijana wenzake wa Timu ya Taifa ya vijana (U20) huko nchini Eritrea na wakafanikiwa kutwaa medali ya dhahabu katika michuano iliyoandaliwa na CECAFA


Gazeti la michezo la Mwanaspoti lilimtaja Samatta kuwa Mchezaji Bora wa Tanzania anayecheza nje ya nchi. Hiyo ilikuwa katika msimu wa 2012/13


Wengi walimfahamu Samatta akiwa African Lyon ambako alifanya mambo makubwa hadi kuwatamanisha Wekundu wa Msimbazi Simba. Msimu wake wa mwisho akiwa Lyon, Samatta alionyesha uwezo mkubwa ikiwemo kufunga mabao mengi hadi klabu hiyo ikaamua kumtunukia Medali hii maalum


Kwa uzalendo alionao kwa taifa lake, ndani ya kabati hilo Samatta ameweka 'Scarf' ya bendera ya Taifa huku akieleza kuwa anajivunia sana kuwa Mtanzania
Akiwa TP Mazembe, Samatta alifanikiwa kufunga 'Hattrick' tatu, na hii hapa ndio mipira aliyoondoka nayo huko DR Congo. Hata hivyo straika huyo anasikitika kupotelewa na mpira mmoja ambao alikabidhiwa baada ya kupiga Hattrick akiwa Simba SC

Post a Comment

 
Top