BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa
NAHODHA wa Manchester United​Wayne Rooney amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kuwa hatajiunga na timu yoyote ya Uingereza na ana matumaini ya kustaafu akiwa na Mashetani hao wa Old Trafford.

Rooney alijunga na United miaka 12 iliyopita akitokea Everton na kufanikiwa kushinda mataji matano ya ligi na moja la klabu bingwa barani Ulaya huku akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu ya Uingereza mwaka 2010. 

Rooney pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza ambayo ipo Ufaransa kushiriki michuano ya Euro ambayo itaanza kesho ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kufanya vyema katika mashindano hayo kutokana na kujituma kwake.

Licha ya kuwa mpambanaji ndani ya uwanja lakini pia Rooney ni kiongozi mzuri kwa wachezaji wenzake ndani na nje ya uwanja hivyo mara nyingi amekuwa akiwapa morali kufanya vizuri.

United wamepata kocha mpya Jose Morinho na katika Wachezaji ambao wanampa kiburi Mreno huyo ni Rooney.

Post a Comment

 
Top