BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya Vijana ya Shelisheli, inatarajiwa kuingia nchini kesho saa 7.45 usiku kwa ajili ya mchezo dhidi ya  ‘Serengeti Boys’ utakaofanyika Juni 26,   saa 10.00 jioni katika Uwanja wa Taifa jijini  Dar es Salaam.

 Timu hiyo inaingia na wachezaji pamoja na viongozi 25 kwa ujumla wake na itafikia hoteli ya Southern Sun iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.

 Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo huo wa kimataifa ambao matokeo ya ushindi ndiyo yatakayoisaidia Serengeti Boys kuwa na nafasi ya kusonga mbele katika michuano hiyo. 

Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.

 Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.

Mechi ya marudiano itapigwa nchini Ushelisheli Julai 2.

Post a Comment

 
Top