BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
Picha kwa hisani ya Global Publishers

YANGA ilianza mazoezi yake jana kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria huku wakiendelea na usajili wa kukiimarisha kikosi chao.

BOIPLUS ilihudhuria mazoezi ya leo ambayo yalifanyika katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam na kushuhudia kocha mkuu Hans Van Pluijm akiwasisitiza wachezaji wake kucheza mpira wa kasi huku wakipiga pasi fupi fupi.

Baada ya mazoezi hayo beki Ramadhan Kessy alisema "Ni siku yangu ya pili tu hapa lakini nimeona utofauti mkubwa, huyu kocha anaonyesha hataki mchezo, ukileta mchezo anakubadilikia kweli.

" Ngoja kikosi kitimie ndio nitaweza kuelezea nafasi yangu kikosini hapo, si umeona pale tulikuwa hatujatimia," alisema Kessy ambaye msimu uliopita alikuwa Simba.

Kwa upande wake beki Andrew Vicent Vicent 'Dante'  ambaye leo ndio ameanza rasmi mazoezi alikiri kushtushwa utofauti ya ufundishaji wa kocha mzungu na wazawa ambao ndio amewazoea.

"Nimeona utofauti mkubwa sana kuanzia aina ya mazoezi tunayopewa pamoja na usimamizi, naamini hapa nitakuwa na mabadiliko baada ya muda si mrefu." alisema Dante

Yanga wataendelea kufanya mazoezi katika uwanja huo hadi siku watakayoondoka kuelekea nchini Algeria

Post a Comment

 
Top