BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar 

POLISI wa vikosi vya kutuliza ghasia wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wapenzi na mashabiki waliochelewa kufika uwanjani baada ya uwanja kujaa huku wao wakilazimisha kuingia.

Mashabiki waliochelewa wako wengi zaidi ya walioingia ndani kitu kinachowapa kazi ya ziada Askari hao na kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Hali hiyo imetokea baada ya uongozi wa Yanga kufuta viingilio vya mchezo huo huku wakitakiwa na shirikisho la mpira wa miguu CAF kuingiza mashabiki 40,000 pekee ambapo uwezo wa uwanja unapokea watu 60,000.

Tayari mageti yote ya uwanja wa Taifa yamefungwa tangu saa sita mchana baada ya uwanja kujaa.

BOIPLUS itaendelea kukujuza kila kinachoendelea toka hapa uwanja wa Taifa.

Post a Comment

 
Top