BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa
TIMU ya Taifa ya Uingereza usiku huu imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Urusi katika mchezo mgumu wa michuano ya UEFA EURO 2016, mechi hiyo ilichezwa kwenye dimba la Stade Velodrome.

Kipindi cha kwanza kilimalizika bila mashabiki kushuhudia bao lolote zaidi ya kosa kosa kadhaa zilizotokea pande zote mbili.

Kipindi cha pili Uingereza walikuwa wa kwanza kupachika bao ambapo katika dakika ya 73, mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Eric Dier ulitinga nyavuni moja kwa moja.


Ikionekana kama vile Waingereza wangeyaanza vema mashindano hayo, nahodha wa Urusi, Denis Glushakov alifunga bao la kusawazisha kwa kichwa na kuwakata maini maelfu ya mashabiki wa Uingereza waliohudhuria mchezo huo.

Hizi hapa ni baadhi ya picha za matukio mbalimbali yaliyotokea katika mchezo huo. Beki kisiki wa Urusi, Igor Smolnikov akimtuliza Raheem Sterling


 Mashabiki wa Uingereza wakiruka uzio kuwakimbia mashabiki wa Urusi waliokuwa wakiwafuata

 Wachezaji wa Urusi wakimpongeza Glushakov baada ya kuisawazishia timu yao

 Wzlinzi wa Uingereza wakiutazama mpira wa kichwa uliopigwa na Glushakov ukitinga nyavuni

a
 Sehemu ya mashabiki wa Uingereza wakifuatilia mchezo kati ya Timu yao na Urusi

 Walinzi wa Urusi wakizuia shuti la nahodha wa Uingereza, Wyne Rooney

Post a Comment

 
Top