BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda Kwa Msaada Wa Mitandao
KINAPOFIKIA kipindi cha usajili mambo mengi huzungumzwa kama tetesi za nyota mbalimbali kuzihama timu zao na kusajiliwa na timu nyingine. BOIPLUS itakuwa ikikukusanyia tetesi zote kutoka pande mbalimbali na kukuwekea pamoja.

                    Gonzalo Higuain

1. HIGUAIN ANUKIA LIVERPOOL
Baada ya kusambaa kwa picha inayomuonyesha kocha wa Liverpool Jurgen Klopp akiwa ameketi jirani na kaka wa Gonzalo Higuain ambaye pia ni meneja wake, katika mchezo kati ya Argentina na Chile, mashabiki wa Liverpool wameshawishika kuamini raia huyo wa Argentina atamwaga wino

2. BARCA, PSG WAMNYATIA COUTINHO
Gazeti la MARCA la nchini Hispania limeandika kuwa Barcelona na PSG ziko kwenye vita ya kupata saini ya mbrazili, Coutinho huku Barca wakiamini atatengeneza muunganiko mzuri na Neymar.

Tayari Liverpool walishaipiga chini ofa ya paundi 30 Milioni iliyotolewa na PSG huku wakiamini nyota huyo (23) ana thamani kubwa zaidi.

                       Jamie Vardy

3. VARDY 'IN', WALCOTT 'OUT'
Wakati Arsenal wakifanya kila liwezekanalo kumnasa mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy ambaye yupo nchini Ufaransa kwenye michuano ya EURO, Wagonga nyundo West Ham tayari wameshaulizia upatikanaji wa mshambuliaji wa muda mrefu wa Washika bunduki hao, Theo Walcott.

Kwa mujibu wa gazeti la Evening Standard, West Ham wapo tayari kutoa dau linalokadiriwa kufikia Paundi 25 Milioni huku ikisemeka wakala anayeshughulikia 'dili' la Vardy ndiye huyo huyo anafuatilia uhamisho wa Walcott.

4. CONTE AMTAKA KANTE

Kocha mpya wa Chelsea Antonio Conte anajiandaa kumpa ofa ya mkataba wa miaka mitano kiungo 'jembe' wa Leicester, N'Golo Kante ili kuwazima PSG wanaomtolea macho.

                     Robert Lewandowsky

5. ZIDANE ANATAKA WATATU TU
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ametanga kuwawinda wachezaji watatu ambao anaamini akiwapata basi Madrid itakuwa moto wa kuotea mbali. Amemtaja beki wa kushoto wa Bayern Munich, David Alaba, kiungo wa Juventus Paul Pogba na straika Robert Lewandowsky

Post a Comment

 
Top