BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Dar


SHIRIKISHO la soka nchini Tanzania TFF leo limebariki uchaguzi wa klabu ya Yanga ambao umekumbwa na sintofahamu kadhaa kwa takribani mwezi mmoja sasa.

Katika kikao hicho Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikutana na sekretarieti ya Yanga na ile ya TFF kuzungumzia mustakabali wa Uchaguzi wa Yanga.

TFF pia imeiagiza kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo kuwaruhusu wagombea waliochukua fomu TFF kushiriki uchaguzi huo bila kuwekewa vikwazo ili jambo hilo liishe kwa amani.

Baada ya Baraza la Michezo Tanzania BMT kutangaza tarehe ya uchaguzi huo kuwa ni Juni 25, kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo ilitangaza Juni 11 kuwa ndiyo siku ya uchaguzi.

Tayari klabu ya Yanga inaendelea na mchakato wa uchaguzi huku kampeni zikianza rasmi leo. Ifuatayo ni orodha ya wagombea wa nafasi mbalimbali katika katika uchaguzi huo.

Post a Comment

 
Top