BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Tanzania 'Twiga Stars' Nasra Juma ametangaza majina ya wachezaji 23 kitachoingia kambini siku chache zijazo.

Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda Julai 15, kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Wanawake ya Rwanda ikiwa ni mwaliko maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (Ferwafa).

Wakati Ferwafa likiingiza mchezo huo wa Julai 17 kwenye orodha ya michezo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira na Miguu la Kimataifa (Fifa), Rais wa nchi hiyo Paul Kagame atautumia mtanange huo kama sehemu ya burudani  mbele ya wageni wake ambao ni wakuu mbalimbali wanaounda Umoja wa Nchi za Afrika (AU) ambao watakuwa na mkutano wao nchini Rwanda.

Mbali ya soka kama burudani, pia Rais Kagame atatumia mchezo huo kama hamasa kwa wakuu wa nchi ili kutoa kipaumbele kwenye soka la wanawake ambako kwa sasa ni ajira ambayo inakwenda sambamba na kuitikia wito wa kupambana na changamoto za malengo ya milenia (MCC) ambayo pia yanataka wanawake wapate nafasi.

KIKOSI KAMILI NI KAMA IFUATAVYO:

Makipa:
Fatma Omary,Belina na Julius Najiat Abbas

Walinzi:
Stumai Abdallah, Fatma Issa, Anastazia Antony, Happiness Henziron pamoja na Maimuna Khamis

Viungo:
Donisia Daniel,Amina Ali, Amina Ramadhani, Fatuma Bashiri
Wema Richard, Fadhila Hamadi
Mwajuma Abdallah,Anna Hebron pamoja na Sophia Mwasikili

Washambuaji:
Tumaini Michael,Johari Shaaban, Fatma Idd, Shelder Bonifdace, Mafuru Asha,  Saada Rashid na 
Mwanakhamisi Omar

Post a Comment

 
Top