BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa

WENYEJI wa michuano ya UEFA EURO 2016, timu ya Taifa ya Ufaransa wameianza vema michuano hiyo baada ya kuitandika Romania mabao 2-1 kwenye dimba la Stade de France.

Ufaransa walianza kupata bao katika dakika ya 56 lililowekwa nyavuni na straika wa Arsenal, Olivier Giroud akimalizia kwa kichwa krosi ya Dimitri Payet.

Katika dakika ya 64 beki wa Ufaransa, Patrice Evra alimfanyia madhambi mshambuliaji wa Romania, Stanciu katika eneo la 18 hivyo mwamuzi akaamuru ipigwe penati iliyowekwa nyavuni na Stancu.

Payet ndiye aliyeihakikishia Ufaransa pointi tatu muhimu baada ya kufumua shuti kali la mguu wa kushoto lililojaa moja kwa moja nyavuni.

Video za mabao yote zinapatikana kwenye ukurasa wetu wa Instagram @boiplus_blogspot

Post a Comment

 
Top