BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa
TIMU ya Taifa ya Uingereza imerejesha matumaini ya kusonga mbele katika michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wales katika mchezo wa kundi B uliofanyika uwanja wa Bolleart.

Gareth Bale aliipatia Wales goli la kuongoza dakika ya 42 kwa mpira wa adhabu baada ya nahodha Wayne Rooney kufanya madhambi mbele kidogo ya mduara wa kati.

Kipindi cha pili Uingereza ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Jammie Vardy na Daniel Sturridge kuchukua nafasi za Harry Kane na Rahim Sterling hali iliyopelekea kubadilisha hali ya mchezo na kufanikiwa kushinda.

Vardy aliisawazishia Uingereza dakika ya 56 baada ya Rooney kupiga mpira wa adhabu na kumgonga Ashley Williams kisha kumkuta mfungaji akiwa na golikipa pekee.

Sturidge alipeleka furaha kwa 'Three lions' baada ya kuifungia goli la ushindi dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kucheza pasi nyingi ndani ya eneo la hatari la Wales.

Uingereza inaongoza kundi B ikiwa na alama 4 ikifuatiwa na Wales yenye alama tatu huku Urusi wakiwa na moja na Slovakia hawana kitu.

Post a Comment

 
Top