BOIPLUS SPORTS BLOG

Paris, Ufaransa

MATAIFA matatu yamefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 2016 baada ya kushinda michezo yao ya 16 bora inayoendelea nchini Ufaransa.

Katika mchezo wa awali Poland iliwatoa Uswisi kwa mikwaju ya penalti 6-5 baada ya kutoka sare ya goli 1-1. Jacub Blasczykowski aliipatia Poland goli la kuongoza dakika ya 39 kabla ya Xhedan Shaqiri kusawazisha kwa goli safi la 'kideoni'.

Katika mchezo wa pili timu ya Wales inayoongozwa na mchezaji ghali duniani Gareth Bale walipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ireland ya Kaskazini. Mchezaji Gareth McAuley alijifunga mwenyewe katika jitihada za kuokoa mpira uliopigwa na Bale.


Mchezo wa mwisho ulikuwa kati ya Ureno na Croatia uliopigwa katika dimba la Stade Felix Bollaert na kushuhudia vijana wa kocha Fernando Santos wakipata ushindi wa goli 1-0 katika muda wa nyongeza. Shukrani kwa goli la 'jioni' la Ricardo Quaresma dakika ya 118 na kuwafanya Wareno wenye mchezaji bora mara tatu wa dunia Cristiano Ronaldo kufuzu hatua ya robo fainali.

Michuano hiyo inaendelea tena hii leo ambapo wenyeji Ufaransa watashuka dimbani dhidi ya Ireland huku Ujerumani ikicheza na Slovakia, mchezo wa mwisho utakuwa ni kati ya Hungary na Ubelgiji.

Post a Comment

 
Top