BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa
THAMANI ya mshambuliaji wa Leicester City anayewindwa na Arsenal, Jamie Vardy imepanda na sasa anapatikana kwa dau la pauni milioni 30.

Mwandishi anayeheshimika wa kituo cha Sky Italia, Gianluca Di Marzio ameandika  katika  website yake  kuwa, awali mshambuliaji huyo alikuwa anapatikana kwa dau la pauni milioni 22 na sasa imeongezeka kwa pauni milioni 10. 

Kocha wa Arsenal,  Arsene Wenger aliripotiwa kufanya Mawasiliano na Leicester City mwanzoni mwa mwezi Juni lakini kuongezeka kwa dau hilo kunaweza kukamfanya Mfaransa huyo kutafuta mchezaji mbadala.


"Ndiyo maana Wenger alitaka kumsajili kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016 sababu alikuwa anajua thamani yake ingepanda kwa pauni milioni 10 katika dau lake na yeye kutokuwa tayari kutoa kiasi hicho cha fedha," ilisema taarifa hiyo.

Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 29  alitokea benchi na kuisawazishia Taifa lake dhidi ya Wales katika ushindi wa magoli 2-1 katika michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa.

Msimu uliopita Vardy iliifungia timu ya Leicester City magoli 24 katika michezo 36 ya ligi kuu ya Uingereza.

Post a Comment

 
Top