BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI wa Mabingwa wa soka nchini Uingereza Leicester City, Jamie Vardy amekwea pipa na kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya michuano ya EURO.

Inasemekana Vardy alitaka kukamilisha uhamisho wake kwenda Arsenal kabla timu hiyo haijaondoka lakini mambo yamekuwa tofauti na sasa hatma ya mkali huyo wa mabao itafahamika baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.

Vardy alionekana mwenye tabasamu alipoweka 'pozi' kupiga picha ya pamoja na kikosi cha Uingereza dakika chache kabla ndege haijaruka kwenye Uwanja wa ndege wa Luton.


Tayari mshambuliaji wa Arsenal, mfaransa Olivier Giroud ameelezea kufurahishwa kwake na usajili huo huku akiamini kama utafanikiwa basi atatengeneza pacha nzuri na Vardy.

"Nimeambiwa Jamie anataka kujiunga nasi, hiyo ni habari njema sana.

"Naamini tutatengeneza muunganiko mzuri, ni mchezaji bora, tutafurahi kuwa naye," alisema Giroud

Post a Comment

 
Top