BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
 Straika wa TP Mazembe Thomas Ulimwengu (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa Yanga, Kelvin Yondan


 Dansi iliendelea huku Yondan akihakikisha Ulimwengu haondoki eneo hilo


 Yondan akashtuka kuwa Ulimwengu anaweza kuunyanyua mpira huo, hivyo akaamua kuficha mikono nyuma .....lakini 'hapiti mtu hapa'


 Sehemu ya pili ya filamu yao ilianzia hapa baada ya Ulimwengu kupokea mpira mrefu kutoka kwa Salif Coulibaly na kuanza kukimbia huku Yondan akiwa jirani yake


Kasi ya Ulimwengu ikamshinda Yondani


 Yondan akaamua kumzuia straika huyo kwa mikono hadi alipomwangusha nje kidogo ya eneo la 18 na refa kuamuru upigwe mpira wa adhabu mdogo


 Yondan akimlaumu Ulimwengu ambaye alilalamika kuwa ameangushwa ndani ya eneo la 18


Mwamuzi Janny Sikazwe akamwonyesha kadi ya manjano Yondan

Post a Comment

 
Top