BOIPLUS SPORTS BLOG

NAPOLI, Italia
WAKALA wa nyota wa​ Slovakia  Marek Hamsik amekaririwa akisema kuwa mchezaji huyo ataendelea kusalia Napoli licha ya tetesi zinazoendelea kuwa atajiunga na  Chelsea au Manchester United.

Timu zote zilionesha nia ya kumtaka mchezaji huyo mwenye miaka 28 tangu miezi kadhaa iliyopita huku akiwa katika kiwango bora kwenye michuano ya  Euro 2016. Pamoja na hayo wakala wake Juraj Venglos amekanusha haraka taarifa za mchezaji huyo kujiunga na miamba hiyo ya Uingereza.

Venglos ameiambia ​Radio Crc: "Hamsik tayari yupo kwenye klabu kubwa haoni sababu ya kuondoka.

"Siku chache zijazo nitakutana na Rais  Aurelio De Laurentiis na Mkurugenzi wa michezo  Cristiano Giuntoli, lakini siwezi kuzungumzia mustakabali wa nyota huyo ila hawezi kwenda popote."

Wakati huo huo Hamsik mwenyewe akizungumza na ​Sky Italia, alisema ataongeza mkataba wa kuendelea kubaki na hafikirii kwenda mahali popote. 

“Naipenda hii jezi, siku zote nimekuwa nikisema hivyo, bado nina miaka mitano zaidi ya kuendelea kubaki hapa, nina furaha na nitaebdelea kuwepo,” alisema Hamsik.

Hamsik alionyesha kiwango kizuri katika ushindi wa magoli 2-1 wa nchi yake dhidi ya Urusi na Jumatatu atakiongoza kikosi hicho kumenyana na Uingereza katika muendelezo wa michuano ya Euro.

Post a Comment

 
Top