BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
MAREFA wa Morocco wameteuliwa
kuchezesha mechi ya ufunguzi ya hatua
ya makundi ya Kombe la Shirikisho la
Soka Afrika, kati ya wenyeji Mouloudia
Olympique Bejaia na Yanga SC ya
Tanzania Juni 19, mwaka huu.

Mchezo huo wa Kundi A utafanyika
Uwanja wa Unite Maghrebine mjini
Bejaia, Algeria utachezeshwa na
Bouchaib El Ahrach atakayepuliza
kipyenga akisaidiwa na washika
vibendera, Redouane Achik na Youssef
Mabrouk.

Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea
Dar es Salaam kuwakaribisha mabingwa
wa Afrika, TP Mazembe Juni 28 katika
mchezo wake wa pili wa Kundi A.
Na katika mchezo huo, Shirikisho la Soka
Afrika (CAF) limechanganya marefa
kutoka nchi tatu tofauti, ambao ni Janny
Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi,
akisaidiwa na washika vibendera Jerson
Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe
O'michael wa Eritrea.

Timu nyingine katika Kundi A ni
Medeama ya Ghana ambayo itafungua
dimba na TP Mazembe mjini Lubumbashi
Juni 17, mwaka huu, mchezo ambao
utachezeshwa na marefa wa Shelisheli
Bernard Camille, Hensley Danny
Petrousse na Eldrick Adelaide.

Post a Comment

 
Top