BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally
JUMLA ya wagombea 15 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu wa klabu ya Stand United huku wagombea wanne wakiitaka nafasi ya Mwenyekiti, uchaguzi huo umepangwa kufanyika Juni 26 mjini Shinyanga.

Mapema wiki hii Kamati ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti, wakili Paul Kaunda ilitangaza mchakato mzima wa uchaguzi huo na kuanza kutoa fomu kwa wagombea huku zoezi hilo la uchukuaji na urudishaji wa fomu limefungwa rasmi leo.

Wagombea waliojitokeza nafasi ya Mwenyekiti ni Emmanuel Kaombwe, Dr Elson Maeja, Salum Kitumbo na Ibrahim Mbogo wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti aliyechukuwa fomu ni mgombea mmoja pekee, Luhende Richard.

Nafasi za wajumbe waliochukuwa fomu wapo 10 lakini watano ndiyo watakachaguliwa na wanachama wao kwa kupigiwa kura ambao ni Miriam Rukandizya, Jackline Isaro, Godfrey Tibakyenda, Fransisko Magoti na Twahil Njoki.

Wajumbe wengine waliochukuwa fomu ni Steven Mihambo, Albert Silwimba, Ally Maganga, Jimrod Mayanga ma Charles Shigino.

Post a Comment

 
Top