BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON, Uingereza

KOCHA wa ​Arsenal mzee Arsene Wenger anapewa nafasi  kubwa ya kurithi mikoba ya Roy Hodgson ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza. 

Wenger amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na washika bunduki hao huku akifikiria kuachana nao baada ya kumalizika kandarasi hiyo mwakani katika majira ya joto.

Uingereza wapo tayari kusubiri hadi mwakani kumchukua Mfaransa huyo kukinoa kikosi chao ambacho kimepoteza ubora wake uliokuwa nao siku za nyuma.

Kocha huyo mwenye miaka 66 ametumia karibu miaka  20 kuwatumikia Washika Bunduki hao huku Maofisa wa Uingereza wakiona kuwa ndiye chaguo sahihi.

Mkurugenzi mtendaji wa chama cha soka cha Uingereza FA Martin Glenn alipozungumza na vyombo vya Habari baada ya kuondolewa katika michuano ya Euro 2016 alisema wanatakiwa wapate kocha mpya kabla ya kuanza kwa mechi za kufuzu kombe la dunia mwezi Septemba na akapendekeza apatikane kocha wa kigeni.

Post a Comment

 
Top