BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KIKOSI cha mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga kinatarajia kuondoka siku ya Ijumaa nchini Uturuki kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Mo Bejaia Juni 16 au 17.

Yanga waliweka kambi ya muda mfupi nchini Uturuki kwa ajili ya kuwavutia kasi Waalgeria hao katika mchezo wa ugenini ambao wanatakiwa kufanya vizuri ili kujiwekea mazingira mazuri katika mechi zake zinazofuata.

Meneja wa timu hiyo Hafidh Saleh ameiambia BOIPLUS kwa njia ya mtandao kuwa maandalizi ya mchezo yamekamilika kwa asilimia kubwa huku wakifanya mazoezi asubuhi na usiku kwa kuwa mechi yao itapigwa usiku nchini Algeria.

"Kambi inaendelea vizuri, wachezaji wana morali kubwa na wametuhakikishia ushindi katika mchezo ulio mbele yetu," alisema Hafidh.

Aidha Hafidh alisema hakuna mchezaji ambaye amepata majeruhi kitu ambacho kinampa kocha kuwa na wigo mpana wa kuchagua nani wa kucheza katika mtanange huo.

Baada ya mtanange huo Yanga itarejea nyumbani kujiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Juni 28 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top