BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Dar
MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Yanga wameendelea kuimarisha kikosi chao kwa kufanya usajili mpya na kuwapa mikataba mipya wachezaji wao wa zamani ambao bado wana umuhimu kikosini na leo jioni Mbuyu Twite kasaini mkataba wa miaka miwili.

Mbali na Twite inadaiwa kuwa kipa wao Ally Mustafa 'Barthez' naye ameongezwa mkataba mpya na hivyo kuwa na walinda mlango wanne, Deo Munishi, Beno Kakolanya aliyemwaga wino jana pamoja na Benedictor Tonoco anayedaiwa kuwa atapelekwa kwa mkopo timu nyingine ya ligi kuu.

Yanga pia imejitoa muhanga kumkata mchezaji wao wa kigeni kutoka Niger, Issoufou Boubacar Garba ambaye tayari amepewa barua yake ya kuachwa huru kwasababu ameshindwa kumshawishi kocha wake Hans Pluijm juu ya kiwango chake tangu wamsajili.

Mpaka sasa Yanga imenasa wachezaji wanne wapya ambao ni Hassan Kessy, Juma Mahadhi, Beno na Andrew Vincent 'Dante'.

Post a Comment

 
Top