BOIPLUS SPORTS BLOG

ANTALYA, Uturuki
MABINGWA wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga waliopiga kambi nchini Uturuki wanafanya mazoezi usiku kujiandaa  na mchezo wao dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria utakaochezwa usiku nchini Algeria wiki ijayo.

Mabingwa hao watateremka dimbani  kati ya Juni 16,17 au 18 kumenyana na Waalgeria hao kulingana na kalenda ya CAF katika hatua ya nane bora ambayo ina makundi mawili yenye timu nne kila moja.


Yanga waliondoka nchini Jumapili iliyopita kuelekea nchini Uturuki kuweka kambi ya muda mfupi kwa ajili ya michuano hiyo ya kombe la shirikisho ambayo wamefanya vizuri hadi kufikia hatua hiyo.

Baada ya mchezo huo Yanga watarudi nyumbani kuwasubiri TP Mazembe katika mchezo wao wa pili utakaofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Juni 28.

Post a Comment

 
Top