BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS,Ufaransa
BAADA ya kumkosa straika wa Leicester City Jamie Vardy klabu ya Arsenal  sasa imehamia kwa nyota mwingine wa mabingwa hao, Riyard Mahrez anayehusishwa na kujiunga na Washika bunduki wa London kwa ada ya pauni 50 milioni.

Mahrez mwenye umri wa miaka 25 ni miongoni mwa wachezaji wa mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza waliofanya vizuri msimu uliopita na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi PFA.

Wakala wake Kamel Bengougam alikuwepo uwajani kushuhudia mchezo ulioisha kwa sare ya goli 1-1 katika ya Arsenal na Lens jana Ijumaa na kuibua tetesi za kuwa nyota huyo yuko mbioni kujiunga na Washika bunduki hao.

Nyota huyo wa Algeria pia alikuwa akihusishwa na kujiunga na miamba ya soka barani Ulaya zikiwemo timu za Chelsea na Barcelona.

Endapo Mahrez atajiunga na Arsenal atakuwa ni mchezaji wa pili wa Leicester kuachana na mabingwa hao baada ya kiungo Ngolo Kante aliyejiunga na Chelsea.

Post a Comment

 
Top