BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

KUELEKEA kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu ya Vodacom, mshambuliaji mpya wa maafande wa JKT Ruvu Atupele Green aliyetokea Ndanda FC ya mkoani Mtwara amechimba mkwara kuwa hajaenda kwa maafande hao kupumzika bali kupiga kazi ili wasijutie kumsajili.


Atupele ambaye alimaliza msimu uliopita akiwa katika kiwango bora sasa ataungana na kocha Malale Hamsini aliyekuwanaye Ndanda msimu uliopita ameonyesha kujiamini kuwa mabadiliko ya timu hayawezi kuzima moto wake.


Akizungumza na BOIPLUS straika huyo mwenye nguvu alisema "Tupo katika maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi lakini bado hatujapata mechi ya kujipima nguvu kwakuwa kocha wetu mkuu alikuwa anashiriki kozi ya Ukocha.


"Maandalizi haya yananipa matumaini ya kufanya vizuri, naamini nitatisha tu msimu ujao."


Kocha Malale atajiunga na Maafande hao kesho baada ya kumaliza kozi ya leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la mpira barani Afrika hatua ya kwanza ambayo ilikamilika jana chini ya usimamizi wa TFF.


Mshambuliaji huyo ndiye aliyeibuka kinara wa ufungaji katika michuano ya kombe la FA baada ya kufunga magoli matano msimu uliopita.


Msimu uliopita Maafande hao walikuwa wakinolewa na kocha Abdallah Kibaden 'Mputa' ambaye aliweka wazi kutoendelea nao baada ya kufanikiwa kuwanusuru na janga la kushuka daraja.

Post a Comment

 
Top