BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu, Dar
NYOTA wa Kimataifa ya Zimbabwe, Bruce Kangwa, ametua nchini jioni ya leo kwa ajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC ya jijini Dar es Salaam.

Kangwa anatokea kwa vinara wa Ligi Kuu nchini humo, Highlanders FC na mpaka sasa ligi hiyo ikiwa mapumzikoni baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza, amefanikiwa kuwa kileleni kwa ufungaji akiwa na mabao saba.Mzimbabwe huyo ameshachezea timu yake ya Taifa mechi 20 na mpaka sasa yupo kwenye kikosi hicho huku akimudu kucheza nafasi tatu tofauti uwanjani, beki wa kushoto, winga wa kushoto na mshambuliaji.


Picha kwa Hisani ya Azam FC

Post a Comment

 
Top