BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu

KLABU ya Azam FC imeonyesha kupendezwa na huduma ya Wahispaniola na sasa wamemleta Daktari mpya kutoka nchini humo, Sergio Soto Perez kwa ajili ya kuwaganga wanandinga wa Wana lamba lamba hao wenye makazi yao Chamazi jijini Dar es Salaam.

Mtaalamu huyo wa viungo vya wachezaji alipokelewa na Meneja wa Azam, Luckson Kakolaki, aliyeambatana na Kocha Mkuu, Zeben Hernandez.

Perez ataungana na jopo la madaktari wengine wa Azam FC, ambao ni Juma Mwimbe na Twalib Mbaraka, wanaoendelea kutoa matibabu kwa wachezaji wa timu hiyo.

Azam walilifumua benchi lao la ufundi lililokuwa chini ya Muingereza Stewart Hall na kuwaajiri makocha toka nchini Hispania kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kuelekea kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu mwezi ujao.

Post a Comment

 
Top