BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

KOCHA wa Majimaji Kali Ongala yuko mbioni kujiunga na klabu nyingine inayoshiriki ligi Tanzania bara baada ya kuachana na Wanalizombe.

Mkataba wa Ongala na Wanalizombe umemalizika mwishoo

ni mwa msimu uliopita huku viongozi wa klabu hiyo wakiwa kimya kuzungumza kuhusiana na kandarasi mpya ya mchezaji huyo wa Azam FC.

Ongala ameiambia BOIPLUS kuwa jioni ya leo atakutana na mabosi hao wapya kuhusu kujiunga na timu hiyo ambayo atainoa kuanzia msimu ujao lakini alishindwa kuweka wazi kila kitu hadi hapo mpango huo utapofanikiwa.

"Ni kweli kuna timu kadhaa zimeonesha nia ya kunihitaji lakini hii moja ndiyo tutakutana leo kufanya makubaliano kabla ya kusaini kandarasi," alisema Ongala.

Aidha Ongala alisema hawezi kurudi kufundisha Majimaji kutokana na kushindwa kufanya maandalizi ya msimu ujao mapema kitu ambacho kitampa wakati mgumu mwanzoni mwa msimu.

Kocha huyo alisema pia alikuwa akihitaji wachezaji watano ndani ya kikosi hicho lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika huku msimu  mpya ukitarajiwa kuanza mwezi ujao.

"Nilikuwa nahitaji wachezaji watano kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya timu lakini uongozi upo kimya ligi ipo njiani kuanza sasa  mazingira kama hayo sitoweza kurudi tena," alimaliza Ongala ambaye ni mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Dr. Remmy Ongala.

Post a Comment

 
Top