BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
KUMEKUCHA Msimbazi, baada ya mkutano mkuu wa wanachama wa Simba kuridhia mabadiliko, mfanyabiashara aliyetangaza nia ya kuwekeza katika klabu hiyo Mohamed Dewji 'Mo' amewaita viongozi awakabidhi fungu la usajili.

BOIPLUS ambayo imejitega kila eneo kuhakikisha inapata kila kinachoendelea kuhusiana na mchakato huu imezinyaka za chini ya 'kapeti' kuwa Mo anataka kutimiza haraka ahadi yake aliyoitoa siku ya Ijumaa iliyopita.

"Kulikuwa na kikao kwa Mo muda mfupi uliopita,  amemwagiza mtu wake wa karibu awatafute viongozi wa Simba ili awape hela za usajili kabla dirisha halijafungwa. Na anataka waende kamati ya utendaji yote ili awakabidhi kama alivyoahidi Ijumaa," kilifafanua chanzo chetu ndani ya mchakato huo.

Pia bilionea huyo amewataka viongozi hao waende na nyaraka za maamuzi ya mkutano mkuu wa leo juu ya ofa yake aliyotoa ya kuweka kiasi cha sh 20 bilioni ili apewe hisa za 51%.

Post a Comment

 
Top