BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu,Dar
SIKU chache baada ya kurejea uwanjani kutoka majeruhi mshambuliaji Malimi Busungu amejipanga kurejesha makali yatakayomfanya kocha Hans Va Pluijm ampange katika kikosi cha kwanza.

Busungu ambaye aliwahi kuichezea Mgambo JKT ya Tanga ameshindwa kufua dafu mbele ya washambuliaji Amissi Tambwe na Donald Ngoma ambao ndo wamekuwa wakianza kikosi cha kwanza.

Mshambuliaji huyo ameiambia BOIPLUS kuwa amejipanga kikamilifu kuwaonesha wanayanga kuwa hawajakosea kumsajili kutoka Mgambo msimu wa mwaka 2014/15.

"Ligi ikianza nitarudi kwa kasi kubwa ili nipate nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza na uwezo huo ninao," alisema Busungu.

Aidha Busungu alisema pia licha ya timu kutopata mapumziko baada ya kushiriki michuano ya kimataifa lakini bado wataendelea kupambana ili kutetea ubingwa wao.

"Hatujapumzika kabisa tangu kumalizika kwa ligi ila bado tutaendelea kupambana kutetea taji letu msimu huu," aliongea Busungu kwa kujiamini.

Yanga itashuka dimbani Agosti 12 katika mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho dhidi ya MO Bejaia katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top